ZITTO KABWE
Rapper kutoka mji kasoro bahari
[MOROGORO],
AFANDE SELE "THE KING" ametoa shukrani zake kwa Mbunge wa
KIGOMA, TANZANIA Mh. Zitto Kabwe kupelekea msaada aliompatia ...
AFANDE ambae hivi sasa anatamba na ngoma yake ya
DINI TUMELETEWA ambayo amempa shavu msanii
Belle 9 mapema masaa machache yaiyopita kupitia ukurasa wake wa Facebook ameonekana akitoa shukrani zake za dhati kwa
Mh. Zitto Kabwe kwa kuweza kugharamia gharama zote zitakazotumika kwenye utengenezaji wa video ya ngoma yake hiyo ...
Hiki ndicho alichokiandika kupitia ukurasa wake huo, soma hapa chini ...
Afande Sele "The King"Lengo
la hii kazi yangu mpya DINI TUMELETEWA ni kumrudisha mwafrika kwenye
uafrika wake ambao msingi wake ni UMOJA, USHIRIKIANO NA UPENDO. Ambao
kwa siku za hivi karibuni tumeshuhudia ukitoweka. Tumeona
mapigano/mauaji ya itikadi za kidini wenyewe kwa wenyewe, pia kuelezea
uhuru wa kuabudu kwa imani yoyote bila kuvunja sheria za Taifa letu. Kwa
mtu yoyote makini mwenye mapenzi mema kwa Taifa letu na
AFRIKA hawezi kupingana na hilo, kwa kutambua hilo MH; ZITTO ZUBERI
KABWE(ZZB) kajitolea kugharamia gharama zote kwa ajili ya kufanikisha
vidio bora kabisa ya wimbo huu, hii ni kazi yetu wote mimi na wewe,
tunasema asante sana kwa Mh; Zitto. AMANI NA UPENDO KWANZA"
No comments:
Post a Comment