Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji wa Clouds Media Group, Ruge
Mutahaba akiongelea mbele ya waandishi wa habari leo kwenye Hoteli ya
Serena
Kwa upande wake Alaine, amesema amefurahia kuja kupanda kwenye jukwaa la Fiesta na atawapa mashabiki wake burudani kali.
“Ninafuraha kugawama upendo wangu, muziki wangu na nguvu yangu, itakuwa
kali sana. Na nimefurahi kuwa pamoja na wasanii hawa wenye vipaji na
kujifunza zaidi kuhusu Tanzania na kuhusu muziki wenu,” alisema Alaine.
Naye Davido alisema kabla ya kuja Tanzania alikuwa akipata ujumbe mwingi
kutoka kwa mashabiki wake wa hapa waliomuuliza atakuja lini na hivyo
amefurahi kupata wasaa huo.
Mheshimiwa Temba akizungumza
Kuanzia Kushoto: Shilole, Christian Bella, Davido, Alaine pamoja na Meneja Masoko wa Serengeti Premium Lager, Alan Chonjo
Akiongea kwenue mkutano huo uliohudhuriwa na wasanii wa nyumbani pia
wakiwemo Chege, Temba, Shilole na Linah, Mkurugenzi wa Vipindi na
Uzalishaji wa Clouds Media Group, Ruge Mutahaba alisema badala ya kuleta
msanii mmoja mkubwa kutoka Marekani, awamu hii wameamua kuleta wasanii
wengi zaidi ili kuleta ladha nyingi kwenye jukwaa moja.
Alaine na Linah wakijadili jambo. Katikati ni Davido







No comments:
Post a Comment