Pages

Friday, July 18, 2014

FAHAMU KUHUSU NDEGE YA MALAYSIA ILIYOANGUKA

WAASI UKRAINE KURUHUSU WACHUNGUZI
Waasi wa wanaounga mkono Urusi, mashariki mwa Ukraine wataruhusu wachunguzi wa kimataifa kwenda katika eneo ambalo ndege ya Malaysia imeanguka.
Waasi hao wameahidi kulinda eneo hilo ili kuruhusu miili ya watu waliokufa kuchukuliwa, limesema shirika la usalama na ushirikiano la Ulaya. Ndege hiyo ikiwa na watu 295 ilianguka katika eneo linalodhibitiwa na waasi siku ya Alhamisi.
Pande mbili zinazohasimiana nchini Ukraine zimekuwa zikituhumiana kwa kuidungua ndege hiyo kwa kombora.
Ndege hiyo aina ya Boeing 777 ilikuwa ikisafiri kutoka Amsterdam kwenda Kuala Lumpur.
Ilianguka kati ya Kransi Luch katika eneo la Luhansk na Shaktarsk karibu na eneo la Donetsk.
Shirika la ndege la Malaysia limesema ndege hiyo namba MH17 ilikuwa na raia 154 wa Uholanzi, 27 wa Australia, 43 wa Malaysia (wakiwemo wafanyakazi 15 wa ndege) 12 wa Indonesia na Waingereza 9.
Abiria wengine ni raia wa Ujerumani, Ubelgiji, Ufilipino na Canada.
Hili ni janga la pili kulikumba shirika la ndege la Malaysia mwaka huu. Ndege namba MH370 ilipotea wakati ikitokea Malaysia kwenda China mwezi Machi, na bado haijapatikana mpaka leo.






No comments:

Post a Comment