Pages

Tuesday, November 8, 2016

Zlatan Ibrahimovic ataikosa mechi dhidi Arsenal Nov 19

 Mchezaji wa klabu ya Man United Zlatan Ibrahimovic ataikosa mechi dhidi Arsenal Nov 19, baada ya jana katika mchezo dhidi ya Swansea kupata kadi ya njano ya 5 msimu huu.

 Msweden huyo alipata kadi ya njano ya kwanza msimu huu kwenye mechi dhidi ya Man City Sept,10 na nyingine akipata walipocheza dhidi ya Stoke, Liverpool, Man City (EFL Cup) na ya tano dhidi ya Swansea.
Zlatan alipata kadi hiyo kunako dk ya 76 baada ya kumchezea vibaya Leroy Fer , na matokeo yake atakosa mechi dhidi ya washika bunduki wa London itakayopigwa Old Trafford mara baada ya mapumziko ya mechi za kimataifa.

No comments:

Post a Comment