Advertise with us here... Contact: 0654 264 472 Email: sabanhussein@yahoo.com sabanhussein@yahoo.com

Monday, June 10, 2013

HIVI NDIVYO ILIVYOJIRI NDOA YA H.BABA NA FROLA MVUNGI.

                                                            H Baba na mkewe Flora Mvungi katika pozi.

BAADA ya maneno kibao katika uhusiano wao, hatimaye wasanii wa filamu na muziki Bongo, Hamis Ramadhan Baba ‘H. Baba‘ na Flora Mvungi, wametiza ahadi yao ya kufunga ndoa ya nguvu. 

Wawili hao walifungishwa ndoa na Shehe Maulid katika Msikiti wa Kibo, uliopo Ubungo, Dar, Jumamosi iliyopita na baada ya ndoa kufungwa sherehe ilifanyika nyumbani kwa akina Flora maeneo ya Kibo. 
     
Flora akimnywesha mumewe kinywaji.
Baada ya watu kula na kunywa na maharusi kusaini vyeti vya ndoa, waliondoka kuelekea nyumbani kwao Mikocheni, Dar ambako kulikuwa na sherehe ya maulidi kulikokuwa na vyakula na vinywaji vya kutosha.

 “Tumefurahi sana na tunamshukuru Mungu kwa kuwa tumetimiza ndoto yetu kwani maneno yamesemwa mengi sana juu ya uhusiano wetu lakini Mungu ameendelea kutuweka pamoja mpaka tumefunga ndoa,” alisema Flora.

H Baba akisaini kitabu cha ndoa.

Akizungumza na mwandishi  wetu, H. Baba alifunguka kuwa aliamua kutokufanya sherehe ukumbini kutokana na wazee wake kukataa kwani kwa dini ya Kiislamu hairuhusiwi kufanya sherehe ukumbini ndiyo maana wakaamua kufanya maulidi tu.
 Flora naye akisaini kitabu cha ndoa.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

0 comments:

Post a Comment

Total Pageviews

Popular Posts

Unordered List

http://michuzijr.blogspot.com/2013/03/party-kubwa-ya-pasaka-kudondoshwa.html

Flickr Images

Follow Us

Bin Hussein65 copyright 2014. Powered by Blogger.

Translate

Followers

Search This Blog