MSANII WA ISIDINGO "LETTIE MATABANA" ALIYEISHI KWA VIRUSI VYA UKIMWI TANGU 2011 AFARIKI DUNIA,HII NI INTERVIEW YAKE YA MWISHO.
Muigizaji maarufu wa wa tamthilia ya Isidingo Lesego Motsepe maarufu kama Lettie Matabane, amethibitishwa kufariki dunia jana huko nyumbani kwake Johannesburg, Afrika Kusini majira ya saa saba mchana.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwa niaba ya familia ya Motsepe, kaka yake aitwaye Moemise Motsepe ndiye aliyekuwa wa kwanza kufahamu juu ya kifo cha dada yake Lesego aliyefariki dunia saa tano za asubuhi jana Jumatatu (January 20), na taarifa za kifo chake kutolewa masaa mawili baadaye.
Lesego, 39, aliigiza katika tamthilia ya Isidingo toka mwaka 1998 hadi 2008. Alijitangaza kuwa muathirika wa virusi vya ukimwi katika siku ya ukimwi duniani December 1, 2011 na kwa wakati huo alikiri kuishi na virusi hivyo kwa miaka 13.
Motsepe alisema kuwa sababu ya kukiri kwake hadharani ilikuwa ni kutaka kuleta tofauti katika maisha ya wengine baada ya yeye kupata mateso ya kukanwa na chuki baada ya wale walio karibu yake kufahamu juu ya hali ya yake.
“Virusi vinaishi kwenye damu yangu. Kwa miaka kumi na tatu toka nimejifahamu, na nimetaka kutumia nafasi ambayo Mungu amenipa kuwa mshauri kwa wale ambao watakuwa wanapitia mapambano niliyoyapitia ,” alisema Letti.
0 comments:
Post a Comment