Advertise with us here... Contact: 0654 264 472 Email: sabanhussein@yahoo.com sabanhussein@yahoo.com

Tuesday, June 10, 2014

MZEE SMALL AZIKWA NA MAMIA YA WATU, AACHA LAANA KUBWA...!!! SOMA HAPA UJUE LAANA UNAMUHUSU NANI

 Mwili wa Mzee Small ukiwa kaburini.

HATIMAYE aliyekuwa nguli wa sanaa za maigizo Bongo, Said Ngamba ‘Mzee Small’ amezikwa jana katika Makaburi ya Tabata-Segerea jijini Dar es Salaam hukuakiacha laana kwa tasnia ya maigizo.
Mzee Small alifariki dunia usiku wa kuamkia Jumapili kwenye Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) ambako alilazwa akisumbuliwa na maradhi ya kiharusi yaliyomuanza miaka takriban miwili iliyopita.Wakati wa kuugua kwake, marehemu aliwahi kulalamikia kitendo cha sehemu kubwa wa wasanii wa Bongo Movies kumtenga kiasi cha kuwa ombaomba hali iliyomfanya awe akisema: “Mungu yupo, iko siku.”
“Mzee Small amezikwa sasa, lakini kichwani lile neno lake kwamba Mungu yupo kwa sababu tulikuwa hatumsaidii kwa lolote naliogopa sana,” alisema mmoja wa mastaa wa Bongo Muvi ambaye hakupenda jina lake litoke gazetini.
 Aliendelea: “Unajua yale maneno ya kutulalamikia ambayo yalikuwa ya kweli kabisa, ni laana kwetu wasanii kwani tumekuwa tukibagua watu. Akiumwa fulani mwenye jina kubwa kwa sasa tunakimbilia, akifa fulani mwenye jina kubwa kwa sasa tunakimbilia, lakini wakongwe kama marehemu Mzee Small ameondoka akiwa hana msaada kutoka kwenye tasnia.
“Leo hii ameondoka, nini katuachia kama si laana.
Maana hajaacha faida kwetu ambayo tunaweza kusema tutarithi.”
Wakati wa uhai wake, marehemu Mzee Small alipotembelewa na waandishi wetu, aliwalalamikia wasanii wa filamu nchini akisema: “Mimi nimewafundisha vijana wengi maigizo.
“Pia ni mmoja wa waliohangaikia sanaa mpaka leo hii unaona vijana wana mafanikio, wanaendesha magari nk.
Ni kwa sababu ya sisi tuliotangulia. Leo hii nina matatizo wananikimbia, Mungu yupo.”
Naye mtoto wa marehemu, Mohmud Ngamba alisema mzee wake kabla hajafa alimuonya kutofuata mambo ya dunia na kushika sana njia za Mungu na wawe na upendo kwa watu.

Pia alimwambia ajitahidi kufanya sanaa ili aje kuwa kama yeye baba yake.Nje ya familia ya marehemu anapatikana msanii mwenzake, Chausiku Salum ‘Bi Chau’ ambaye kilio chake baada ya kupokea kifo cha msanii huyo kilikuwa kikubwa kupita watu wengi wa karibu na marehemu.
Bi. Chau alikipokea kifo cha mkongwe huyo wa maigizo akiwa jijini Tanga.

Bi. Chau alianza kuigiza na marehemu miaka ya tisini akiwa kama mke wa kwenye sanaa hali iliyowafanya wengi kuamini ni mke halali wa marehemu hata nje ya jukwaa la sanaa.Katika kipindi cha mateso ya ugonjwa wake, wadau mbalimbali walijitokeza kumsaidia kwa hali na mali huku wito 
mkubwa ukitolewa kwamba, watu zaidi wajitokeze badala ya kusubiri kutoa rambirambi.
Mwenyezi Mungu aiweke pema peponi roho ya marehemu Mzee Small. Amina.Chanzo:Gazeti Uwazi

0 comments:

Post a Comment

Total Pageviews

Popular Posts

Unordered List

http://michuzijr.blogspot.com/2013/03/party-kubwa-ya-pasaka-kudondoshwa.html

Flickr Images

Follow Us

Bin Hussein65 copyright 2014. Powered by Blogger.

Translate

Followers

Search This Blog