MAAJABU YA DUNIA: MIWANI "INAYOSOMA" MAWAZO YAKO, SOMA HAPA.
Miwani ya kisasa ya Google imedukuliwa, ambapo sasa inaweza kufanya kazi kwa kusoma mawazo ya mtu.
Mtumiaji anaweza kupiga picha kwa kufikiria tu.
Kwa kutumia miwani hiyo ya kisasa na kuunganisha kichwani na kifaa kijulikanacho kama electroencephalography (EEG) ambapo kifaa uroro huweza kusoma unachofikiria, na hata kupiga picha bila kujigusa au kubonyeza mahala popote.
Kampuni ya This Place ya London iliyotengeneza kifaa uroro hicho (software) imesema inaweza kutumika pale watu wanapohitaji kufanya mambo mengine bila kutumia mikono yao, mathalan wakati madaktari wanafanya upasuaji.
This Place imetoa kifaa uroro hicho MindRDR bure na wana imani kuwa huenda wataalam wengine wanaweza kutumia kwa shughuli nyingine.
Hata hivyo Google imesema haitambui kifaa uroro hicho.
"Miwani yetu ya Google haiweza kusoma mawazo ya mtu" msemaji wa Google ameiambia BBC.
Kutaka kujaribu kifaa uroro hicho kama una miwani ya Google, ingia:https://github.com/ThisPlace/MindRDR
0 comments:
Post a Comment