Advertise with us here... Contact: 0654 264 472 Email: sabanhussein@yahoo.com sabanhussein@yahoo.com

Monday, January 26, 2015

HII NDIO HALI HALISI YA HALI YA MCHEZAJI WA SIMBA SC EMMANUEL OKWI

Mshambuliaji machachari wa timu ya soka ya Simba, Emmanuel Okwi, jana jioni amenusurika kifo baada ya kupigwa kiwiko nyuma ya kichwa kwenye mishipa ya fahamu na kuzimia kwa dakika kadhaa uwanjani.

Mkasa huo ambao umethibitishwa na daktari wa timu hiyo, Yassin Gembe, ulitokea wakati wa pambano la ligi kuu ya Vodacom baina ya timu hiyo na Azam FC lililopigwa kwenye uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na kuisha kwa sare ya bao 1-1. Bao la Simba lilifunwa na Okwi wakati lile la Azam likiwekwa kimiani na Kipre Tchetche.

Kwa mujibu wa Gembe, Okwi alipatiwa huduma ya kwanza uwanjani hapo kabla ya kupelekwa kwenye zahanati iliyoko pia uwanjani hapo na kisha baadaye kukimbizwa Hospitali ya Rufaa ya Muhimbili kwa matibabu zaidi.

“Ilikuwa mbaya sana na angeweza hata kupoteza maisha,” alisema Gembe na kuongeza;
“Tuliendelea kumpatia matibabu kwenye zahati ndogo uwanjani hapo mpaka aliporejesha fahamu ndipo tukaanza kuelekea Muhimbili kwa matibabu zaidi yaliyochukua takribani masaa mawili. Ila kwa sasa yuko vizuri.”

Hata hivyo kwa mujibu wa taarifa za daktari, Okwi atakuwa nje ya uwanja kwa siku kadhaa wakati akiwa chini ya uchunguzi kuangalia maendeleo ya afya yake. Hiyo ni pamoja na kuwa nje katika ratiba ya mazoezi ya timu hiyo.

0 comments:

Post a Comment

Total Pageviews

Popular Posts

Unordered List

http://michuzijr.blogspot.com/2013/03/party-kubwa-ya-pasaka-kudondoshwa.html

Flickr Images

Follow Us

Bin Hussein65 copyright 2014. Powered by Blogger.

Translate

Followers

Search This Blog