Advertise with us here... Contact: 0654 264 472 Email: sabanhussein@yahoo.com sabanhussein@yahoo.com

Wednesday, August 3, 2016

Msanii wa muziki Shetta amefunguka na kueleza faida alizozipata baada ya kutangaza management yake mpya ambayo imemsaidia kufanya mambo ambalimbali ambayo hapo awali alikuwa akiyafanya mwenyewe.

Akiongea na Bongo5 Jumapili hii, Shetta amesema ameamua kufanya muziki wake ‘kiprofessional’ zaidi tofauti na awali.
“Kuamua kuwa na management ni kuamua kuwa professional, huwezi kuwa msanii huna management, huna mtu ambaye anakupangia ratiba, huna mtu ambaye nasimamia kazi zako, huyo ni uswahili,” alisema Shetta.
Aliongeza, “Ni kitu kizuri lazima uwe professional, yaani haiwezekani mtu akaja akadeal na mimi direct, lazima awasiliane na uongozi, mimi napewa tu taarifa ya mikakati na nini kifanyike,”
Pia rapper huyo ambaye anafanya vizuri na wimbo ‘Namjua’ amewataka mashabiki wa muziki wake kusubiria surprise za kazi mpya

0 comments:

Post a Comment

Total Pageviews

Popular Posts

Unordered List

http://michuzijr.blogspot.com/2013/03/party-kubwa-ya-pasaka-kudondoshwa.html

Flickr Images

Follow Us

Bin Hussein65 copyright 2014. Powered by Blogger.

Translate

Followers

Search This Blog