Advertise with us here... Contact: 0654 264 472 Email: sabanhussein@yahoo.com sabanhussein@yahoo.com

Thursday, October 27, 2016

Bila skendo siku hizi huchomoki kimuziki – Matonya

Baada ya muda mrefu kupita na jina la Matonya kutoonekana miongoni mwa majina yanafanya vizuri katika muziki wa Bongo Flava kama ilivyokuwa miaka kadhaa iliyopita, hatimaye mkali huyo kutoka Tanga ameibuka na kudai kuwa mabadiliko ndio yamemfanya asisikike.
Matonya aliongea hayo nilipofanya naye mazungumzo maeneo ya Kinondoni jijini Dar. Alidai kuwa sasa hivi ili kazi yako ionekane nzuri lazima uwe na tatizo na mtu au skendo kubwa kitu ambacho yeye binafsi hajakizoea na kumfanya ashindwe kwendana na mfumo huo wa sasa.
“Mabadiliko ambayo yamebadilika sasa hivi ukitoa kazi nzuri lazima uwe na tatizo au uwe na scandal kubwa ambayo wengine hatujazoea kufanya hivyo vitu kwahiyo wengine tumejaribu kuuza muziki wetu bila ya scandal,” alisema.
Matonya amedai kuwa ubora wake kimuziki bado uko pale pale na wale wanaojua muziki mzuri wameendelea kumuunga mkono. Kwa sasa Matonya ana wimbo na video mpya, Sugu Benchi.
By Edward Fabian

Related Posts:

0 comments:

Post a Comment

Total Pageviews

273511

Popular Posts

Unordered List

http://michuzijr.blogspot.com/2013/03/party-kubwa-ya-pasaka-kudondoshwa.html

Flickr Images

Follow Us

Bin Hussein65 copyright 2014. Powered by Blogger.

Translate

Followers

Search This Blog