Janet Jackson kumpatia jina la ‘Michael’ mtoto wake wa kwanza
Janet Jackson na mumewe Wissam Al Mana wanadaiwa kupanga kumpatia jina la Michael mtoto wao wa kwanza.
Wawili hao wamepanga kumpatia mtoto wao huyo anayetarajiwa kuzaliwa mwezi ujao jina hilo kwa madai kuwa ni kumuenzi mfalme wa muziki wa Pop duniani, marehemu Michael Jackson pamoja na kuleta upendo kwenye familia yao.
Mpaka sasa ni miaka saba imepita tangu kilipotokea kifo cha Michael Jackson, Juni 2009.
Taarifa za Janet kuwa na ujauzito zilianza kusambaa mwezi Mei, mwaka huu lakini muda wote muimbaji huyo hakuzungumza chochote mpaka pale alipoamua kufunguka kwa mara ya kwanza kwenye tovuti ya People mwezi huu.
0 comments:
Post a Comment