Advertise with us here... Contact: 0654 264 472 Email: sabanhussein@yahoo.com sabanhussein@yahoo.com

Thursday, October 27, 2016

Mwanariadha wa Kenya Rita Jeptoo aongezewa adhabu ya miaka 2 kutoshiriki mchezo huo

Mwanariadha kutoka Kenya, Rita Jeptoo ameongezewa adhabu ya miaka miwili zaidi kutoshiriki mchezo huo kutokana na tuhuma za kutumia dawa za kusisimua misuli.
Uamuzi huo uliopitishwa na mahakama ya kutatua mzozo katika michezo Switzerland, unazima matumaini kwa mwanariadha huyo kurudi mchezoni katika miaka ya hivi karibuni.
Mshindi huyo wa mara tatu wa mbio za Boston marathon alishindwa katika rufaa aliyokata kupinga kuongezwa muda wa miaka hiyo miwili uliokuwa ukitarajiwa kumalizika mwishoni mwa mwezi huu.
Wito wa kuongeza marufuku hiyo ulitolewa katika kesi dhidi yake na shirikisho la kimataifa la riadha IAAF.
Rita Jeptoo alipatikana na hatia ya kutumia dawa hizo za kusisimua misuli na shirikisho la riadha Kenya katika uchunguzi aliyofanyiwa mnamo 2014: alipatikana kutumia dawa ya kushinikiza damu EPO.
Matokeo yake katika mashindano tangu Aprili mwaka huu yamefutiliwa mbali, ikiwemo ushindi wake katika mashindano ya Boston na Chicago marathon alikoibuka nambari moja.
Source: BBC

Related Posts:

0 comments:

Post a Comment

Total Pageviews

273604

Popular Posts

Unordered List

http://michuzijr.blogspot.com/2013/03/party-kubwa-ya-pasaka-kudondoshwa.html

Flickr Images

Follow Us

Bin Hussein65 copyright 2014. Powered by Blogger.

Translate

Followers

Search This Blog