Advertise with us here... Contact: 0654 264 472 Email: sabanhussein@yahoo.com sabanhussein@yahoo.com

Saturday, October 22, 2016

Tecno Phantom itaweza kuchuana na simu vinara duniani?

Soko la simu za mkononi barani Afrika lina maelfu wa watengenezaji ambao wamekua wakishindana kila siku kumiliki soko kubwa. Ushindani mkubwa wa asili uliopo umesababisha ya wauzaji wauzaji kama Trium, Motorola, NEC, Bird, Alcatel na Sagem kupotea.


Wakati nyingi zikififia, huku chache miongoni mwa hizo zinapata wakati mgumu, TECNO inakuwa.
Ingawa kiasi fulani cha wauzaji wa kimataifa kama Nokia, Blackberry, Samsung na Apple bado wanaendelea kuuza bidhaa zao barani Afrika, Nokia na Blackberry wanaonekana kupoteza bahati katika soko kila kukicha kutokana na sababu mbalimbali. Cha kushangaza, katika kipindi hiki ambacho baadhi wanafifia na kupoteza umaarufu, TECNO imefanikiwa kuingia sokoni na katika miaka 10 katika soko imefanikiwa kujijengea jina kubwa barani Afrika.
Bidhaa bora zinapaswa kupatikana kwa bei nafuu
Barani Afrika leo, wauzaji wachache bado wanajitutumua kwa sababu wamefululiza kutoa matoleo mapya yenye teknolojia ya hali ya juu inayopendwa na watumiaji, kwa bahati mbaya yanauzwa kwa kwa gharama kubwa sana. Kweli, hicho kinatakiwa kuwa kipimo cha kuuzwa kwa bei kubwa? TECNO haikubalianai na hilo, kila mwaka, simu zenye teknolojia ya hali ya juu kama matoleo ya Phantom zimeingia katika soko zikiwa na sifa za ubunifu wa hali ya juu, muonekano mzuri na teknolojia ya juu zaidi kwa bei ya kuridhisha.


TECNO iko nafasi gani kutoka simu bora zaidi duniani?
Kwa upande wa kuwafikia watu, ni dhahiri TECNO inayapita makampuni makubwa yanayoongoza barani Afrika, lakini haiku hivyo katika maeneo mengine duniani na pengine hii inasababishwa na ukweli kwamba hawajishughulishi na masoko ya huko. Lakini kwa upande wa ubora wa bidhaa, matoleo ya TECNO Phantom yana ushindani wa kutisha kama simu nyingine zenye teknolojia ya hali ya juu hivyo uchaguzi wa mteja utategemea sana uaminifu na unafuu wa bidhaa ikiwa ni moja ya eneo ambalo TECNO iko poa kulinganisha na nyingine.





Unaweza kutembelea kurasa za mitandao ya kijamii ya Tecno kufahamu zaidi kuhusiana na Tecno Phantom 6
Facebook
Instagram
Twitter

Related Posts:

0 comments:

Post a Comment

Total Pageviews

273580

Popular Posts

Unordered List

http://michuzijr.blogspot.com/2013/03/party-kubwa-ya-pasaka-kudondoshwa.html

Flickr Images

Follow Us

Bin Hussein65 copyright 2014. Powered by Blogger.

Translate

Followers

Search This Blog