Mimi
ni Jane naishi mwenge Dar es salaam naomba utalifuta jina la baba yangu
maana sitaki liwe kwenye blog watu watanijua na kuniangamiza maana
nimeshawaangamiza wengi sana kwa UKIMWI ila mengine yote usifute hata
moja ili dunia ijue tu japokua mimi nitakufa kwa huu ukimwi nilionao.
Nilizaliwa mkoa wa Dodoma na nilishi vizuri
tu tangu utotoni na hata sikujihusisha na ngono hadi nilipomaliza form 4
mwaka 2006 baada ya kumaliza nilikuja hapa Dar kuishi kwa mama mdogo
aliyeolewa hapa Mwenge.
Nilipata marafiki wengi tu na kuna kijana
mmoja alinitongoza kwa muda mrefu sana na siunajua vijana wengi hutumia
muda mrefu kutongoza ili msichana unadhani kwamba labda huyo anakupenda
kumbe anataka tu ngono na wadada wengi sana hudhani kufuatiliwa kwa muda
mrefu na mvulana basi huyo yuko serious kumbe hakuna lolote.
Nilimkubalia tukawa wapenzi ila nilikataa
kuhusu kufanya mapenzi maana anayekupenda kiukweli sio uongo lazima
asitake ngono kabla ya ndoa.
Kwa miezi kama 5 hadi 6 aliniambia kuhusu
kufanya mapenzi nilikataa alitumia mbinu nyingi sana kwa kunibembeleza
na hata kulia mbele yangu ili tufanye tu mara moja ila nilikataa,
alisema atavumilia hadi siku ya ndoa yetu ambapo tulipanga kuoana mwaka
sept 2009.
Siku moja aliniambia twende kwenye kumbi za
starehe na mimi kwa sababu ya upagani na kumwamini pia kwa sababu
nampenda nilikubali tulienda huko na kulikua na bendi fulani maarufu ya
mziki wa dansi ilikua inatumbuiza.
Tulitafuta sehemu na kukaa na mpenzi wangu
akaagiza pombe alianza kunywa huku akinionjesha, nilikataa kwa sababu
nilikua sijawahi kunywa pombe katika maisha yangu yote, hata sijui
alinishawishi vipi nilijikuta nakunywa kidogo kidogo na kwa kuwa tulikaa
pale kwa muda zaidi ya masaa 5 nadhani nikunywa kama bia 3 au 4 japokua
nilikua nakunywa kidogo kidogo tu tena kwa kunywesha na mpenzi wangu
maana nikama nikua nanyweshwa kila baada kama ya dakika 25 ndipo
nakunywa mara moja na sikujuia kama nakunywa pombe ila niliihisi tu
naonja ili kumlizisha mpenzi wangu.
Ilipofika saa 10 alfajiri nilihisi usingizi
na pia nilijiona wa tofauti najua nililewa hata kama sikujua kama
nimelewa maana nakumbuka tulitoka pale huku amenishika mkono huyo mpenzi
wangu. Tulikodo tax na kuondoka na siku hiyo aliniambia twende kwake
alikokua amepanga chumba maana tulikua na usingizi sana nilikubali huku
nikidhani hatuwezi kufanya mapenzi.
Tulifika salama na kuingia ndani ukweli
pombe ni kichocheo cha ngono na ningekua mimi ndio Raisi wa Tanzania
ningefunga bar zote. Nilijikuta natamani kufanya mapenzi na huyu mpenzi
wangu hata alikua hana nia maana alijua atanichukiza sana na uhusiano
ungekufa siku hiyo lakini kwa sababu ya pombe nilimwambia siku hiyo
tufanye kidogo maana mwili wangu unataka.
Ni kweli siku hiyo kwa sababu ya pombe
nilifanya mapenzi na huyo mpenzi wangu na baadae akanipeleka nyumbani
baada ya wiki mbili maana tulikaa wiki mbili bila kuonana alikuja na
kunieleza habari ambayo sikuihitaji katika maisha yangu maana nilikua
nasikia tu kwa watu wengine lakini sio kwangu alisema ”JANE ISHI KWA
MATUMAINI KUANZIA SASA”
Nilidhani utani lakini aliniambia kuwa yeye ana UKIMWI tangu miaka mitano iliyopita na anapenda tu ngono maana hawezi kuacha.
Nililia sana na baada ya wiki moja baadae
nikaenda kupima na kukutwa nina ugojwa ambao niliusikia tu kwa watu na
chanzo cha yote ni pombe, kupenda starehe,disko na upagani unaotusumbua
wanadamu wengi.
Nilikua na UKIMWI na kwa hasira maana
mpenzi wangu alihamia Arusha huku akisema neno moja la mwisho kwamba
”shetani amemtuma kuwaambukiza wanadamu UKIMWI”
Sikujua, sikujua, sikujua, sikujuaaaaaaaaa,
basi tu ooh YESU nihurumie mimi leo.Nilibebeshwa mzigo ambao
haukunistahili mimi. Hata leo hua najiuliza kwamba nilijitunza kwa miaka
23 yote lakini pombe na huyu wakala wa shetani wamenifanyia hivi. Baada
ya kujua nina UKIMWI na hali hiyo nikaikubali na kulikua na kundi kubwa
sana la wanaume ambao walikua wamewahi kunitongoja na niliwakataa sana
kwa sababu hii niliwakubali ili nami nife na wengi.
Nilianza kumkubali kila mmoja na kuna baba
mmoja ambaye ana wake 3 niliwahi kumtukana sana kipindi cha nyuma kila
aliponitongoza lakini wakati huu nilimkubali na hakuamini na tukafanya
ngono tena bila kinga na akaniaachia pesa laki 6 kama zawadi ya
kumkubali kumbe naye hakujua kuwa namwambukiza na hata leo hua
nawahurumia tu wale wake zake ambao wana UKIMWI uliotoka kwangu.
Kiukweli tangu may 2009 hadi 2012
nimeshatembea na wanaume zaidi 1500 maana ilifika kipindi nala na
wanaume 3 kwa siku na lengo langu niwakomeshe kama mimi nilivyokomeshwa
na nina uhakika kutokana na mimi wameambukizwa UKIMWI wanadamu zaidi ya
10,000 na hili tangazo la ”TUKO WANGAPI” huwa linaniliza kila siku maana
hata mimi najua kabisa nilianzisha mtandao kama huo wa ngono kwa idadi
kubwa sana ya watu.
Nimeokoka miezi 7 iliyopita na siku
naombewa nilikutwa na mapepo mengi sana na hata waombeaji wakashangaa.
Ningejua ningeokoka tangu nikiwa na miaka 5 lakini ndio hivyo sina jinsi
wala uwezo wa kubadirisha hali hiyo.
Na naomba kila atakayesoma ujumbe huu ajue
kuanzia leo kuwa pombe ni dhambi pia kwenda disko ni dhambi,kuuza pombe
ni dhambi na kila kichochoe chochote cha dhambi ni dhambi. Hadi sasa mtu
yeyote hawezi kujua kama nina UKIMWI na sijui MUNGU ana mpango gani na
mimi maana kwake yote yanawezekana. Nauamini uponyaji wake na sijawahi
kutumia ARV hata siku moja na afya yangu iko sawa tu na huwezi hata wewe
kujua kama uovu huu nimefanya mimi.
Ndugu zangu kama una UKIMWI nenda kanisani
ukaombewe na kama una akili mpe YESU maisha yako maana pia baada ya kifo
ni hukumu. Yasalimishe maisha yako kwa YESU na usiambukize wengine
tena.
Mimi tangu niokoke sijawahi kufanya mapenzi
tena na sitafanya hivyo wala sitaolewa na mtu yeyote maana yatosha kwa
uovu niliofanya na hadi sasa wapo ninaowajua zaidi ya 15 wameshafariki
na nilihudhulia misibani huku nikijua kabisa chanzo ni mimi.
Mwisho nawashauli wababa kulidhika na wake
zao na wamama pia lidhikeni na waume zenu, vijana ambao hamjaoa wala
kuolewa subiri hadi utakapooa au kuolewa na kabla ya kuolewa au kuoa
kapimeni kwanza kwani wenye UKIMWI ni wengi kuliko unavyozani.
Fuata unachofundishwa kanisani na pia soma BIBLIA na uwe mtakatifu.
MUNGU akubariki
Ni mimi Jane,
Mwenge, Dar es salaam
Tanzania
UKIMWI UPO JAMANI, CHA MSINGI NI TUWE MAKINI.
Tuwe waaminifu, tusubiri au tutumie c
kondom......

No comments:
Post a Comment