Pages

Thursday, July 27, 2017

PICHA: WAZIRI WA AFYA AMEWAPATIA VITAMBURISHO VYA MATIBABU BURE KWA WAZEE KIGAMBONI


leo tarehe 27/7/2017, Waziri wa Afya, Maendeleo ya jamii, Ustawi wa jamii, jinsia na watoto Mhe. Ummi Mwalimu alikuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa vitambulisho vya matibabu bure kwa wazee wa wilaya ya Kigamboni ulifanyika katika viwanja vya hospitali ya Vijibwemi, kigamboni.
Mapema asubuhi leo hii, Mkuu wa wilaya ya Kigamboni Mhe Hashim Mgandilwa, Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigamboni Mhe. Stephen katemba na Mbunge wa Kigamboni Faustine Ndugulile(mb), Madiwani na viongozi mbalimbali walikua wenyeji wakimkaribusha Waziri wa afya katika uzinduzi huo.

Baada ya kumkaribisha Waziri wa afya Mhe. Ummi Mwalimu, Mhe. Hashimu Mgandilwa alimuomba Waziri wa afya kuongeza nguvu katika sekta ya Afya kigamboni kwa kujenga vituo vya afya Zaidi na ikiwezekana kila kata iwe na kituo cha afya katika Kigamboni.
Mkurugenzi wa manispaa ya Kigamboni Ndg Stephen Katemba akitoa taarifa ya utambuzi na utolewaji wa vitambulisho vya matibabu bure kwa wazee, amesema halmashauri yake imekwisha watambua wazee 3000 na kati yao 2374   wamepatiwa vitambulisho hivyo leo huku vingine vikiendelea kutengenezewa

Mbunge wa Jimbo la Kigamboni Mhe Dkt Faustine Ndungulile amekemea vikali vitendo vya baadhi ya wahudumu wa afya kuwatoza pesa akina mama wajawazito na kutaka vitendo hivyo kaachwa mara moja.  Aidha ameongeza kuwa katika Jimbo la Kigamboni hapendi kuona wananchi wanapandishiwa bei za dawa kinyume na utaratibu na wananchi kunyimwa dawa ili wakanunue nje ya hospitali.

Pia alielezea changamoto ya kupatikana kwa kambi ya wazee katika wilaya ya Kigamboni, Changamoto ya upungufu wa watumishi katika manispaa ya Kigamboni na Changamato za Upokeaji na upatikanaji wa dawa Kigamboni. Mhe. Ndugulile ameagiza “Taarifa zote za dawa ziwekwe katika mbao za matangazo, zikiwepo taarifa za tarehe ya kupokelewa mzigo.”

Waziri wa Afya Mhe. Ummi mwalimu wakati akizungumzia changamoto za wakina mama na watoto wakati wa kujifungua amesema “ Gharama za kujifungua nitakata juu kwa juu kutoka katika pesa za manispaa za afya.” Pia amesema  “Tarehe 30 September nitafanya uhakiki katika halmashauri zote. ambazo zitakuwa hazijafanya uhakiki wa wazee kwaajiri ya vitambulisho, nitatangaza kuwa zinamgogoro na wazee.” Alimaliza kwa kusema “Kama tumeweza kutoa elimu bure tutashindwaje kutoka huduma bora za afya kwa mama na mtoto na wazee."

Tukio hilo la Uzinduzi wa vitambulisho vya matibabu bure kwa wazee wa wilaya ya Kigamboni ,limehudhuliwa na  wadiwani wote wa manispaa ya Kigamboni, wazee, watendaji wa Kata na mitaa pamoja na wananchi.

Wazee wa Kigamboni na wananchi wengine pamoja wakifuatilia kwa makini ugawaji wa vitamburisho hivyo


Mmoja wa wazee waliopatiwa vitamburisho akikabidhiwa kitamburisho chake.






 Mhe. Dkt.Faustine ndugulile(mb) kigamboni
 Mkurugenzi kigamboni Mhe. Stephen Katemba 
Moja kati ya wazee waliopatiwa vitambulisho leo na Mhe. Ummi Mwalimu waziri wa Afya akisoma Risala
Mhe. waziri wa afya akizungumza na mgonjwa katika Hospitali ya Vijibweni, Kigamboni.



No comments:

Post a Comment