Pages

Saturday, October 14, 2017

Naibu Waziri Wizara ya Afya Mhe.Faustine Ndugulile “Mhe. Raisi ametupa maelekezo kusimamia na kuhakikisha hakuna ukosefu wa dawa katika huduma za afya.”


Leo tarehe 14/10/2017 Naibu Waziri wizara ya Afya , maendeleo ya jamii, wazeejinsia  na watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile amefanya uzinduzi wa Zanati ya Pemba Mnazi Kigamboni. Zahanati hiyo pamoja na nyumba moja ya mganga zilizojengwa Kigamboni  kata ya Pemba mnazi katika mtaa wa Pemba Mnazi .

Msemaji wa Dhahanati hiyo amesema “Zahanati hiyo imejengwa kwa gharama ya Tsh Milioni 75 na nyumba ya Mgaaga mkuu kwa Tsh milioni 20, imefunguliwa ikiwa na watumishi wawili tu ambao ni Mganga mmoja na Muuguzi mmoja. Pia imepokea vitanda ishirini, magodoro ishirini na vyandarua kutoka kwa Mheshimiwa Rais Dkt. John Magufuli kupitia MSD.”

Aidha msemaji huyo ameelezea  changamoto mbalimbali ikiwemo ya Ukosefu wa  Umeme. Ameendelea kwa kuelezea kuwa tathmini ya gharama ya kufunga umeme wa Sola ni ghari zaidi kuliko umeme wa kawaida(Tanesco) hivyo amemuomba mgeni rasmi kuliangalia hilo. Pia amemuomba sana Mhe. Naibu waziri na Mkurugenzi kuisimamia sana Zahanati hiyo kutokana na kutokuwepo katika bajeti ya fedha  ya 2016-2017, mpaka pale itakapokuwepo katika bajeji ijayo.
Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni

   Mhe. Hashimu Mgandilwa amemkaribisha mgeni rasmi na kutanguliza salamu zake kwa wizara ya Afya na maendeleo ya jamii.  Katika salamu zake hizo amepata nafasi ya kuelezea changamoto zinazoikabiri Wilaya ya Kigamboni katika sekta afya  zikiwemo za Upungufu wa watumishi na magari ya kubebea wagonjwa(Ambulance). Hivyo ameomba wilaya ya Kigamboni kukumbukwa katika mgawanyo wa watumishi na vitendea kazi wa wizara, ili kuendana na kasi ya serikali ya awamu ya tano ya hapa kazi tu na ni katika utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi.

Naibu Waziri wizara ya afya mhe.Faustine Ndugulile amewapongeza Mkuu wa wilaya ya Kigamboni  Mhe. Hashimu Mgandilwa na Mjurugenzi wa manispaa ya Kigamboni Bw. Stephen Katemba kwa usimamizi wao mzuri na ufuatiliaji katika afya wilaya ya Kigamboni. Ameeleza pia alipita kwa kushtukiza kukagua ujezi wa majengo mapya ya Zahanati ya Buyuni, amefurahishwa na kumkuta Mkuruenzi wa Manispaa yupo kule na Tingatinga lake wakiendelea na kazi.
Mhe. Naibu waziri amesema Serikali imeongeza kutoka bilioni 31 mpaka kufikia bilioni 251 mwaka jana, na mwaka huu imeongeza bilioni 11 na kufikifia bajeti ya billion 262 kwa Zahanati na vituo vya Afya. Na amepitia kukagua amekuta dawa zipo za kutosha, amesema hatarajii kusikia mwanachi wa Pemba mnazi akilalamika kwa kukosa dawa.

Aidha Mheshimiwa Naibu wziri amesema Juzi amepata mrejesho kutoka katika watu wa wizara na ameambiwa kuwa vituo vya afya na zahanat izetu Kigamboni tunaoongoza, tumepewa nyota tatu. amewapongeza sana  , kwahiyo ameomba waongeze bidii na kasi kufikia nyota tano na sio kushuka.
Alimalizia kwa kusema “Serikali imetupatia milioni 500 kwa ajiiri ya kujenga chumba cha Upasuaji Kimbiji pamoja na ambulance. Tutajitahidi tuweze kulikamilisha hili mapema.”

Mhe. Naibu Waziri amemuomba Mkurugenzi kumleta meneja wa Tanesco aje kufanya tathmini ya na ikiwezekana Mkurugenzi atoe pesa na kama hazitapatikana mimi nitazitafuta. Meneja aje Jumatatu na mimi nitashirikiana kulisimamia pamoja na ofisi ya wilaya ya Kigamboni. Hata hivyo upatikanaji huduma za Xray ningeomba Mkurugenzi kufikia mwishoni mwa mwaka huu tuwe tumepata, ukitaka wataalamu mimi nitakusaidia kutoka wizarani.

Siku kadhaa zilizopita serikali iliweza kukabishi eneo lililokuwa linajulikana kama shamba la Nafko kwa serikali ya Kigamboni na pale ndipo tutakapojenga hospitali ya Wilaya. Serikali tunaendelea kuimarisha huduma bora kwa kina mama wajawazito na watoto  na pia wazee. Tunataka kuhakikisha wazee wote wanapatiwa vitambulisho vya matibabu bure na tupo katika mkakati wa kuwezesha kila mwananchi awe na Bima ya afya.


                                 Naibu Waziri wizara ya Afya Mhe. Dkt Faustine Ndugulile


Mhe. DAC wilaya ya Kigamboni Raheli Muhando








 Meya wa Manispaa ya Kigamboni Mhe. Maabadi Hoja



Mkuu wa wilaya ya Kigamboni Mhe. Hashimu Mgandilwa
Wananchi wakifuatilia kwa makini mkutano
Meya  wa Manispaa ya Kigamboni ambaye pia ni Diwani wa kata hiyo ya Pemba Mnazi Mhe. Maabadi Hoja alimalizia kwa kushukuru na kuwasisitiza wananchi wa Pemba mnazi kushirikiana na Manispaa ya Kigamboni kuzitunza na kuzisimamia vizuri Zahanati hizo.

No comments:

Post a Comment