Jay Z ajipanga kutoa $40m kununua nyimbo za Prince
Bosi wa mtandao wa Tidal, Jay Z ameanza kujaribu kupata haki miliki ya nyimbo za marehemu Prince aliyefariki mwezi April, mwaka huu.
Kwa mujibu wa mtandao wa TMZ, Jay Z alikutana na mmoja wa ndugu wa Prince, Tyka na kumueleza kuwa yupo tayari kununua haki miliki za nyimbo za Prince ambazo bado hazijatoka kwa kulipa kiasi cha dola milioni 40.
Hata hivyo Tyka hana haki ya kusaini mkataba huo mpaka pale atakapokutana na meneja wa marehemu Prince na baadhi ya ndugu zake wengine wenye haki na nyimbo hizo. Kabla ya kifo chake, Prince aliwahi kuachia nyimbo zake kwenye mtandao wa Tidal lakini pia wawili hao walikuwa na urafiki wa ukaribu.
Jay Z aliwahi kurap kwenye wimbo wa ‘All The Way Up (Remix)’, “Prince left his masters where they safe and sound. We never gonna let the elevator take us down.”
0 comments:
Post a Comment