Advertise with us here... Contact: 0654 264 472 Email: sabanhussein@yahoo.com sabanhussein@yahoo.com

Latest Posts

Thursday, May 24, 2018

Saturday, October 14, 2017

Naibu Waziri Wizara ya Afya Mhe.Faustine Ndugulile “Mhe. Raisi ametupa maelekezo kusimamia na kuhakikisha hakuna ukosefu wa dawa katika huduma za afya.”


Leo tarehe 14/10/2017 Naibu Waziri wizara ya Afya , maendeleo ya jamii, wazeejinsia  na watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile amefanya uzinduzi wa Zanati ya Pemba Mnazi Kigamboni. Zahanati hiyo pamoja na nyumba moja ya mganga zilizojengwa Kigamboni  kata ya Pemba mnazi katika mtaa wa Pemba Mnazi .

Msemaji wa Dhahanati hiyo amesema “Zahanati hiyo imejengwa kwa gharama ya Tsh Milioni 75 na nyumba ya Mgaaga mkuu kwa Tsh milioni 20, imefunguliwa ikiwa na watumishi wawili tu ambao ni Mganga mmoja na Muuguzi mmoja. Pia imepokea vitanda ishirini, magodoro ishirini na vyandarua kutoka kwa Mheshimiwa Rais Dkt. John Magufuli kupitia MSD.”

Aidha msemaji huyo ameelezea  changamoto mbalimbali ikiwemo ya Ukosefu wa  Umeme. Ameendelea kwa kuelezea kuwa tathmini ya gharama ya kufunga umeme wa Sola ni ghari zaidi kuliko umeme wa kawaida(Tanesco) hivyo amemuomba mgeni rasmi kuliangalia hilo. Pia amemuomba sana Mhe. Naibu waziri na Mkurugenzi kuisimamia sana Zahanati hiyo kutokana na kutokuwepo katika bajeti ya fedha  ya 2016-2017, mpaka pale itakapokuwepo katika bajeji ijayo.
Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni

   Mhe. Hashimu Mgandilwa amemkaribisha mgeni rasmi na kutanguliza salamu zake kwa wizara ya Afya na maendeleo ya jamii.  Katika salamu zake hizo amepata nafasi ya kuelezea changamoto zinazoikabiri Wilaya ya Kigamboni katika sekta afya  zikiwemo za Upungufu wa watumishi na magari ya kubebea wagonjwa(Ambulance). Hivyo ameomba wilaya ya Kigamboni kukumbukwa katika mgawanyo wa watumishi na vitendea kazi wa wizara, ili kuendana na kasi ya serikali ya awamu ya tano ya hapa kazi tu na ni katika utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi.

Naibu Waziri wizara ya afya mhe.Faustine Ndugulile amewapongeza Mkuu wa wilaya ya Kigamboni  Mhe. Hashimu Mgandilwa na Mjurugenzi wa manispaa ya Kigamboni Bw. Stephen Katemba kwa usimamizi wao mzuri na ufuatiliaji katika afya wilaya ya Kigamboni. Ameeleza pia alipita kwa kushtukiza kukagua ujezi wa majengo mapya ya Zahanati ya Buyuni, amefurahishwa na kumkuta Mkuruenzi wa Manispaa yupo kule na Tingatinga lake wakiendelea na kazi.
Mhe. Naibu waziri amesema Serikali imeongeza kutoka bilioni 31 mpaka kufikia bilioni 251 mwaka jana, na mwaka huu imeongeza bilioni 11 na kufikifia bajeti ya billion 262 kwa Zahanati na vituo vya Afya. Na amepitia kukagua amekuta dawa zipo za kutosha, amesema hatarajii kusikia mwanachi wa Pemba mnazi akilalamika kwa kukosa dawa.

Aidha Mheshimiwa Naibu wziri amesema Juzi amepata mrejesho kutoka katika watu wa wizara na ameambiwa kuwa vituo vya afya na zahanat izetu Kigamboni tunaoongoza, tumepewa nyota tatu. amewapongeza sana  , kwahiyo ameomba waongeze bidii na kasi kufikia nyota tano na sio kushuka.
Alimalizia kwa kusema “Serikali imetupatia milioni 500 kwa ajiiri ya kujenga chumba cha Upasuaji Kimbiji pamoja na ambulance. Tutajitahidi tuweze kulikamilisha hili mapema.”

Mhe. Naibu Waziri amemuomba Mkurugenzi kumleta meneja wa Tanesco aje kufanya tathmini ya na ikiwezekana Mkurugenzi atoe pesa na kama hazitapatikana mimi nitazitafuta. Meneja aje Jumatatu na mimi nitashirikiana kulisimamia pamoja na ofisi ya wilaya ya Kigamboni. Hata hivyo upatikanaji huduma za Xray ningeomba Mkurugenzi kufikia mwishoni mwa mwaka huu tuwe tumepata, ukitaka wataalamu mimi nitakusaidia kutoka wizarani.

Siku kadhaa zilizopita serikali iliweza kukabishi eneo lililokuwa linajulikana kama shamba la Nafko kwa serikali ya Kigamboni na pale ndipo tutakapojenga hospitali ya Wilaya. Serikali tunaendelea kuimarisha huduma bora kwa kina mama wajawazito na watoto  na pia wazee. Tunataka kuhakikisha wazee wote wanapatiwa vitambulisho vya matibabu bure na tupo katika mkakati wa kuwezesha kila mwananchi awe na Bima ya afya.


                                 Naibu Waziri wizara ya Afya Mhe. Dkt Faustine Ndugulile


Mhe. DAC wilaya ya Kigamboni Raheli Muhando








 Meya wa Manispaa ya Kigamboni Mhe. Maabadi Hoja



Mkuu wa wilaya ya Kigamboni Mhe. Hashimu Mgandilwa
Wananchi wakifuatilia kwa makini mkutano
Meya  wa Manispaa ya Kigamboni ambaye pia ni Diwani wa kata hiyo ya Pemba Mnazi Mhe. Maabadi Hoja alimalizia kwa kushukuru na kuwasisitiza wananchi wa Pemba mnazi kushirikiana na Manispaa ya Kigamboni kuzitunza na kuzisimamia vizuri Zahanati hizo.

Thursday, July 27, 2017

PICHA: WAZIRI WA AFYA AMEWAPATIA VITAMBURISHO VYA MATIBABU BURE KWA WAZEE KIGAMBONI


leo tarehe 27/7/2017, Waziri wa Afya, Maendeleo ya jamii, Ustawi wa jamii, jinsia na watoto Mhe. Ummi Mwalimu alikuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa vitambulisho vya matibabu bure kwa wazee wa wilaya ya Kigamboni ulifanyika katika viwanja vya hospitali ya Vijibwemi, kigamboni.
Mapema asubuhi leo hii, Mkuu wa wilaya ya Kigamboni Mhe Hashim Mgandilwa, Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigamboni Mhe. Stephen katemba na Mbunge wa Kigamboni Faustine Ndugulile(mb), Madiwani na viongozi mbalimbali walikua wenyeji wakimkaribusha Waziri wa afya katika uzinduzi huo.

Baada ya kumkaribisha Waziri wa afya Mhe. Ummi Mwalimu, Mhe. Hashimu Mgandilwa alimuomba Waziri wa afya kuongeza nguvu katika sekta ya Afya kigamboni kwa kujenga vituo vya afya Zaidi na ikiwezekana kila kata iwe na kituo cha afya katika Kigamboni.
Mkurugenzi wa manispaa ya Kigamboni Ndg Stephen Katemba akitoa taarifa ya utambuzi na utolewaji wa vitambulisho vya matibabu bure kwa wazee, amesema halmashauri yake imekwisha watambua wazee 3000 na kati yao 2374   wamepatiwa vitambulisho hivyo leo huku vingine vikiendelea kutengenezewa

Mbunge wa Jimbo la Kigamboni Mhe Dkt Faustine Ndungulile amekemea vikali vitendo vya baadhi ya wahudumu wa afya kuwatoza pesa akina mama wajawazito na kutaka vitendo hivyo kaachwa mara moja.  Aidha ameongeza kuwa katika Jimbo la Kigamboni hapendi kuona wananchi wanapandishiwa bei za dawa kinyume na utaratibu na wananchi kunyimwa dawa ili wakanunue nje ya hospitali.

Pia alielezea changamoto ya kupatikana kwa kambi ya wazee katika wilaya ya Kigamboni, Changamoto ya upungufu wa watumishi katika manispaa ya Kigamboni na Changamato za Upokeaji na upatikanaji wa dawa Kigamboni. Mhe. Ndugulile ameagiza “Taarifa zote za dawa ziwekwe katika mbao za matangazo, zikiwepo taarifa za tarehe ya kupokelewa mzigo.”

Waziri wa Afya Mhe. Ummi mwalimu wakati akizungumzia changamoto za wakina mama na watoto wakati wa kujifungua amesema “ Gharama za kujifungua nitakata juu kwa juu kutoka katika pesa za manispaa za afya.” Pia amesema  “Tarehe 30 September nitafanya uhakiki katika halmashauri zote. ambazo zitakuwa hazijafanya uhakiki wa wazee kwaajiri ya vitambulisho, nitatangaza kuwa zinamgogoro na wazee.” Alimaliza kwa kusema “Kama tumeweza kutoa elimu bure tutashindwaje kutoka huduma bora za afya kwa mama na mtoto na wazee."

Tukio hilo la Uzinduzi wa vitambulisho vya matibabu bure kwa wazee wa wilaya ya Kigamboni ,limehudhuliwa na  wadiwani wote wa manispaa ya Kigamboni, wazee, watendaji wa Kata na mitaa pamoja na wananchi.

Wazee wa Kigamboni na wananchi wengine pamoja wakifuatilia kwa makini ugawaji wa vitamburisho hivyo


Mmoja wa wazee waliopatiwa vitamburisho akikabidhiwa kitamburisho chake.






 Mhe. Dkt.Faustine ndugulile(mb) kigamboni
 Mkurugenzi kigamboni Mhe. Stephen Katemba 
Moja kati ya wazee waliopatiwa vitambulisho leo na Mhe. Ummi Mwalimu waziri wa Afya akisoma Risala
Mhe. waziri wa afya akizungumza na mgonjwa katika Hospitali ya Vijibweni, Kigamboni.



Thursday, April 27, 2017

Mitindo: Namna ya kupatia vazi la ripped jeans

Suruali za jeans ndizo suruali pekee ambazo huvaliwa zaidi na kupendwa na watu wengi duniani.
 Tukizungumzia jeans kwa kipindi hiki basi usisahau kutaja Ripped Jeans(jeans za kuchanwa chanwa), ambazo zinazidi kuvaliwa kila kukicha na watu. Muonekano wa suruali hii unaweza ukakufanya ustaajabu ikiwa bado haijavaliwa na mtu.
 Ripped jeans ama jeans za kuchanwa chanwa inaweza kuvaliwa sehemu yoyote , na ni vizuri ikivaliwa sehemu za burudani kama matamsha ya kimuziki.

 Vjiana ndio asilimia kubwa ya wavaaji wa suruali hizi za kuchanwa chanwa. Mwaka 2011 suruali zilianza kuingia madukani na kuvaliwa. Ingawa ilikua kazi kuwashawishi watu kuvaa jeans hizo, ongezeko la wavaaji linazidi kuongezeka.
 Hata hivyo, suruali hizii hazifai ofisni na mahala pa kazi.
 Zipo Ripped jeans tofauti tofauti yani za watu wenye miili mikubwa( wanene) na wenye miili membamba kwa watu wa jinsia zote.

Fahamu: Samaki zebra anayetibu uti wa mgongo.

Watafiti kutoka Marekani wamebaini aina ya samaki aitwae Zebra Fish, ambaye anaweza kuzalisha upya, uti wake wa mgongo wa mwanadamu unapovunjika.
Watafiti hao wamesema kuwa samaki huyo ana uwezo wa kulizalisha upya uti wa mgongo unapovunjika kwa kuziunganisha kama daraja, sehemu zilizokatika kwa kutumia aina ya protini mwilini mwa samaki huyo.
Binadamu anayo aina hiyo ya protini inayoweza kuzalisha mifupa, lakini haifanyi kazi sawa na ile ya samaki Zebra. Aina hiyo ya protini kwenye binadamu inafanana kwa asilimia 90 na aina hiyo kwenye samaki hao.

Kuwepo kwa mpango wa chanjo kwa umma dhidi ya homa ya uti wa mgongo barani Afrika umepata mafanikio makubwa. Zaidi ya watu milioni mbili wamepata kinga dhidi ya maradhi hayo, kutoka nchi zipatazo 16 barani Afrika, kutoka Gambia mpaka Ethiopia.
Shirika la Afya Duniani limesema katika kipindi cha mwaka 2013, kulikuwa na wagonjwa wanne tu, katika bara hilo ambalo awali, liliweka rekodi ya kuwa na maelfu ya vifo vinavyotokana na ugonjwa huo wa homa ya uti wa mgongo. Kila mwaka, kampeni ya kupambana na ugonjwa huo ilianza mwaka 2010.
wepo wa samaki zebra atasaidia kupunguza ama kuondoa ugonjwa huo duniani kote.

Samatta aisaidia Genk kuwania tiketi ya UEFA mwakani

Mchezaji tegemezi katika kikosi cha timu ya taifa ya Tanzania na klabu ya KRC Genk, Mbwana Ally Samatta, amesaidia klabu yake ya Genk kutoka na suluhu ya goli 1-1 dhidi ya kikosi cha AS Eupen mchezo uliochezwa katika Uwanja wa Kehrweg mjini Eupen, ikiwa ni mchezo wa Kundi B kuwania tiketi ya kucheza michuano ya UEFA Europa League mwakani.
Samatta, ambae hivi karibuni amejikuta akipachikwa jina jipya la utani na wapenzi wa soka nchini lijulikanalo kama 255 Champion, amefanikiwa kucheza dakika zote 90 katika mchezo huo uliochezwa Jumatano usiku na timu yake, KRC Genk ikilazimishwa sare ya 1-1 na wenyeji, AS Eupen.
Klabu ya Genk ilikuwa ya kwanza kupata bao kupitia kiungo wa Ukraine, Ruslan Malinovskiy dakika za awali za mchezo huo, kabla ya wenyeji kuchomoa kwa mkwaju wa penalti kupitia mchezaji Luis Garcia katika kipindi cha pili.
Mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Tanzania Sama Goals alianza katika kikosi hiko baada ya mchezo uliopita wa michuano hiyo kutokea benchi Jumapili ambapo Genk walishinda 6-0 dhidi ya Royal Excel Mouscron, wakiwa nyumbani Uwanja wa Luminus Arena.
Klabu ya Genk inaongoza kundi hilo la B katika mchuano wa kuwania tiketi ya Europa League kwa kuwa jumla ya point 13 ikiwa imecheza mechi Tano huku Mchezaji huyo akiwa ameshatimiza mechi 54 tangu kujiunga na klabu hiyo akitoka katika klabu ya Tp Mazembe ya DRC alikofanikiwa kufunga jumla ya mabao 18.
BY HAMZA FUMO

Total Pageviews

Popular Posts

Unordered List

http://michuzijr.blogspot.com/2013/03/party-kubwa-ya-pasaka-kudondoshwa.html

Flickr Images

Follow Us

Bin Hussein65 copyright 2014. Powered by Blogger.

Translate

Followers

Search This Blog