Naibu Waziri Wizara ya Afya Mhe.Faustine Ndugulile “Mhe. Raisi ametupa maelekezo kusimamia na kuhakikisha hakuna ukosefu wa dawa katika huduma za afya.”
Leo tarehe 14/10/2017 Naibu Waziri wizara ya Afya ,
maendeleo ya jamii, wazeejinsia na watoto
Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile amefanya uzinduzi wa Zanati ya Pemba Mnazi
Kigamboni. Zahanati hiyo pamoja na nyumba moja ya mganga zilizojengwa
Kigamboni kata ya Pemba mnazi katika
mtaa wa Pemba Mnazi .
Msemaji wa Dhahanati hiyo amesema “Zahanati hiyo imejengwa
kwa gharama ya Tsh Milioni 75 na nyumba ya Mgaaga mkuu kwa Tsh milioni 20,
imefunguliwa ikiwa na watumishi wawili tu ambao ni Mganga mmoja na Muuguzi
mmoja. Pia imepokea vitanda ishirini, magodoro ishirini na vyandarua kutoka kwa
Mheshimiwa Rais Dkt. John Magufuli kupitia MSD.”
Aidha msemaji huyo ameelezea
changamoto mbalimbali ikiwemo ya Ukosefu wa Umeme. Ameendelea kwa kuelezea kuwa tathmini
ya gharama ya kufunga umeme wa Sola ni ghari zaidi kuliko umeme wa
kawaida(Tanesco) hivyo amemuomba mgeni rasmi kuliangalia hilo. Pia amemuomba
sana Mhe. Naibu waziri na Mkurugenzi kuisimamia sana Zahanati hiyo kutokana na
kutokuwepo katika bajeti ya fedha ya
2016-2017, mpaka pale itakapokuwepo katika bajeji ijayo.
Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni
Mhe. Hashimu Mgandilwa amemkaribisha mgeni
rasmi na kutanguliza salamu zake kwa wizara ya Afya na maendeleo ya jamii. Katika salamu zake hizo amepata nafasi ya
kuelezea changamoto zinazoikabiri Wilaya ya Kigamboni katika sekta afya zikiwemo za Upungufu wa watumishi na magari
ya kubebea wagonjwa(Ambulance). Hivyo ameomba wilaya ya Kigamboni kukumbukwa
katika mgawanyo wa watumishi na vitendea kazi wa wizara, ili kuendana na kasi
ya serikali ya awamu ya tano ya hapa kazi tu na ni katika utekelezaji wa Ilani
ya Chama cha Mapinduzi.
Naibu Waziri wizara ya afya mhe.Faustine Ndugulile
amewapongeza Mkuu wa wilaya ya Kigamboni
Mhe. Hashimu Mgandilwa na Mjurugenzi wa manispaa ya Kigamboni Bw.
Stephen Katemba kwa usimamizi wao mzuri na ufuatiliaji katika afya wilaya ya
Kigamboni. Ameeleza pia alipita kwa kushtukiza kukagua ujezi wa majengo mapya
ya Zahanati ya Buyuni, amefurahishwa na kumkuta Mkuruenzi wa Manispaa yupo kule
na Tingatinga lake wakiendelea na kazi.
Mhe. Naibu waziri amesema Serikali imeongeza kutoka bilioni
31 mpaka kufikia bilioni 251 mwaka jana, na mwaka huu imeongeza bilioni 11 na
kufikifia bajeti ya billion 262 kwa Zahanati na vituo vya Afya. Na amepitia
kukagua amekuta dawa zipo za kutosha, amesema hatarajii kusikia mwanachi wa
Pemba mnazi akilalamika kwa kukosa dawa.
Aidha Mheshimiwa Naibu wziri amesema Juzi amepata mrejesho
kutoka katika watu wa wizara na ameambiwa kuwa vituo vya afya na zahanat izetu
Kigamboni tunaoongoza, tumepewa nyota tatu. amewapongeza sana , kwahiyo ameomba waongeze bidii na kasi
kufikia nyota tano na sio kushuka.
Alimalizia kwa kusema “Serikali imetupatia milioni 500 kwa
ajiiri ya kujenga chumba cha Upasuaji Kimbiji pamoja na ambulance. Tutajitahidi
tuweze kulikamilisha hili mapema.”
Mhe. Naibu Waziri amemuomba Mkurugenzi kumleta meneja wa
Tanesco aje kufanya tathmini ya na ikiwezekana Mkurugenzi atoe pesa na kama
hazitapatikana mimi nitazitafuta. Meneja aje Jumatatu na mimi nitashirikiana
kulisimamia pamoja na ofisi ya wilaya ya Kigamboni. Hata hivyo upatikanaji
huduma za Xray ningeomba Mkurugenzi kufikia mwishoni mwa mwaka huu tuwe
tumepata, ukitaka wataalamu mimi nitakusaidia kutoka wizarani.
Siku kadhaa zilizopita serikali iliweza kukabishi eneo
lililokuwa linajulikana kama shamba la Nafko kwa serikali ya Kigamboni na pale
ndipo tutakapojenga hospitali ya Wilaya. Serikali tunaendelea kuimarisha huduma
bora kwa kina mama wajawazito na watoto
na pia wazee. Tunataka kuhakikisha wazee wote wanapatiwa vitambulisho
vya matibabu bure na tupo katika mkakati wa kuwezesha kila mwananchi awe na
Bima ya afya.
Naibu Waziri wizara ya Afya Mhe. Dkt Faustine Ndugulile
Mhe. DAC wilaya ya Kigamboni Raheli Muhando
Meya wa Manispaa ya Kigamboni Mhe. Maabadi Hoja
Mkuu wa wilaya ya Kigamboni Mhe. Hashimu Mgandilwa
Wananchi wakifuatilia kwa makini mkutano
Meya wa Manispaa ya
Kigamboni ambaye pia ni Diwani wa kata hiyo ya Pemba Mnazi Mhe. Maabadi Hoja alimalizia
kwa kushukuru na kuwasisitiza wananchi wa Pemba mnazi kushirikiana na Manispaa
ya Kigamboni kuzitunza na kuzisimamia vizuri Zahanati hizo.
0 comments:
Post a Comment