PICHA: WAZIRI WA AFYA AMEWAPATIA VITAMBURISHO VYA MATIBABU BURE KWA WAZEE KIGAMBONI
leo tarehe 27/7/2017, Waziri wa Afya, Maendeleo ya jamii,
Ustawi wa jamii, jinsia na watoto Mhe. Ummi Mwalimu alikuwa mgeni rasmi katika
uzinduzi wa vitambulisho vya matibabu bure kwa wazee wa wilaya ya Kigamboni
ulifanyika katika viwanja vya hospitali ya Vijibwemi, kigamboni.
Mapema asubuhi leo hii, Mkuu wa wilaya ya Kigamboni Mhe
Hashim Mgandilwa, Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigamboni Mhe. Stephen katemba na
Mbunge wa Kigamboni Faustine Ndugulile(mb), Madiwani na viongozi mbalimbali walikua
wenyeji wakimkaribusha Waziri wa afya katika uzinduzi huo.
Baada ya kumkaribisha Waziri wa afya Mhe. Ummi Mwalimu, Mhe.
Hashimu Mgandilwa alimuomba Waziri wa afya kuongeza nguvu katika sekta ya Afya
kigamboni kwa kujenga vituo vya afya Zaidi na ikiwezekana kila kata iwe na
kituo cha afya katika Kigamboni.
Mkurugenzi wa manispaa ya Kigamboni Ndg Stephen Katemba
akitoa taarifa ya utambuzi na utolewaji wa vitambulisho vya matibabu bure kwa
wazee, amesema halmashauri yake imekwisha watambua wazee 3000 na kati yao 2374 wamepatiwa vitambulisho hivyo leo huku vingine
vikiendelea kutengenezewa
Mbunge wa Jimbo la Kigamboni Mhe Dkt Faustine Ndungulile
amekemea vikali vitendo vya baadhi ya wahudumu wa afya kuwatoza pesa akina mama
wajawazito na kutaka vitendo hivyo kaachwa mara moja. Aidha ameongeza kuwa katika Jimbo la
Kigamboni hapendi kuona wananchi wanapandishiwa bei za dawa kinyume na
utaratibu na wananchi kunyimwa dawa ili wakanunue nje ya hospitali.
Pia alielezea changamoto ya kupatikana kwa kambi ya wazee
katika wilaya ya Kigamboni, Changamoto ya upungufu wa watumishi katika manispaa
ya Kigamboni na Changamato za Upokeaji na upatikanaji wa dawa Kigamboni. Mhe. Ndugulile
ameagiza “Taarifa zote za dawa ziwekwe katika mbao za matangazo, zikiwepo taarifa
za tarehe ya kupokelewa mzigo.”
Waziri wa Afya Mhe. Ummi mwalimu wakati akizungumzia
changamoto za wakina mama na watoto wakati wa kujifungua amesema “ Gharama za
kujifungua nitakata juu kwa juu kutoka katika pesa za manispaa za afya.” Pia
amesema “Tarehe 30 September nitafanya
uhakiki katika halmashauri zote. ambazo zitakuwa hazijafanya uhakiki wa wazee
kwaajiri ya vitambulisho, nitatangaza kuwa zinamgogoro na wazee.” Alimaliza kwa
kusema “Kama tumeweza kutoa elimu bure tutashindwaje kutoka huduma bora za afya
kwa mama na mtoto na wazee."
Tukio hilo la Uzinduzi wa vitambulisho vya matibabu bure kwa
wazee wa wilaya ya Kigamboni ,limehudhuliwa na
wadiwani wote wa manispaa ya Kigamboni, wazee, watendaji wa Kata na
mitaa pamoja na wananchi.
Mmoja wa wazee waliopatiwa vitamburisho akikabidhiwa kitamburisho chake.
Mhe. Dkt.Faustine ndugulile(mb) kigamboni
Mkurugenzi kigamboni Mhe. Stephen Katemba
Moja kati ya wazee waliopatiwa vitambulisho leo na Mhe. Ummi Mwalimu waziri wa Afya akisoma Risala
Mhe. waziri wa afya akizungumza na mgonjwa katika Hospitali ya Vijibweni, Kigamboni.
0 comments:
Post a Comment