WEMA SEPETU AMWOKOA KAJALA KUTUMIKIA KIFUNGO CHA MIAKA 5 JELA
KAJALA
Wema Sepetu
HUKUMU ya kesi iliyokuwa inamkabili staa wa
filamu za Kibongo, Kajala Masanja na mumewe imetolewa leo na Hakimu
Sundi Fimbo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar. Katika
hukumu hiyo Kajala amehukumiwa kwenda jela miaka mitano au kulipa faini
ya shilingi milioni 13 na mumewe kwenda jela miaka mitano au kulipa
faini ya shilingi milioni 213.
Kajala alikuwa anakabiliwa na kesi ya kuuza
nyumba iliyowekwa kizuizini na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa
(Takukuru) baada ya mumewe, Faraji Agustino kukumbwa na msala wa
kutakatisha fedha haramu.
hata hivyo msanii Wema
Sepetu amemwokoa Kajala kwa kumlipia faini ya shilingi milioni 13 ili kumnusuru na
kifungojela
0 comments:
Post a Comment