Author: Bin Hussein Photography |
11:53 PM |
|
STAA
wa filamu za Kibongo, Jacqueline Wolper Massawe anadaiwa kutupiwa nje
na baadaye kuzuiliwa vyombo vyake kwenye ile nyumba ya kifahari ya
kupanga aliyokuwa akiishi Mbezi Beach, Dar es salaam. Madai hayo yalitua
kwenye dawati la GPL hivi karibuni ambapo ilielezwa kuwa ishu hiyo
ilijiri maeneo hayo baada ya bishosti huyo kudaiwa kuwa alishindwa
kulipa kodi ya pango ya mwezi mmoja ambayo ni Dola 1,500 (zaidi ya Sh.
milioni 2.4 za madafu). Kwa mujibu wa ‘sosi’ wetu aliyekuwepo eneo la
tukio, Wolper aliwatuma ndugu zake kwenda kuchukua vyombo hivyo lakini
walipofika mama mwenye nyumba (jina tunalo), aliwazuia na kumpigia simu
staa huyo akimwambia kuwa anatakiwa kulipa fedha kabla ya kuchukua vitu
vyake. “Wolper alipopigiwa simu alikuja juu na kumwambia mama mwenye
nyumba kuwa kama anamfuatilia eti atamfunga kama mume wa mama huyo
alivyofungwa na kumwambia kuwa atampelekea polisi wakamkamate,” alidai
mtu huyo. Sosi huyo aliendelea kudai kuwa baada ya kuona soo limekuwa la
kutishana, mama huyo alikwenda kumfuata mjumbe wa nyumba kumi
aliyefahamika kwa jina moja la Musa na kumueleza kisha kumuomba asimamie
zoezi hilo. Baada ya kujazwa data hizo, GPL ilifanya jitihada za
kumsaka Wolper na alipopatikana alisema kuwa hajawahi kudaiwa na huyo
mama na anayesema hivyo huenda alimuona wakati anahamisha vitu vyake
kwani kwa sasa amehama kwenye nyumba hiyo. Mwandishi wetu hakuishia
hapo, alimtafuta shemeji wa mama mwenye nyumba aliyetajwa kwa jina moja
la Jamal ambaye alikiri kutokea kwa ishu hiyo na kwamba suala hilo
lilimalizika ambapo vyombo vya Wolper vilitolewa kwa ajili ya kufanya
usafi kwani kuna mtu mwingine alikuwa akihamia. Mjumbe wa Nyumba Kumi,
Musa alipotafutwa kwenye simu yake ya kiganjani ili kuzungumzia sakata
hilo alikiri kufikishiwa malalamiko ya Wolper. Alisema kuwa msanii huyo
alikuwa hajamaliza kulipa fedha, akawatuma
ndugu zake wakachukue
vitu vyake lakini kabla hawajavichukua mama mwenye nyumba aliwazuia
mpaka alipwe chake na alipotimiza hilo ndipo akaachiwa vitu vyake
#Crdt kwa GPL & BONGO NEWS MAGAZINE
TOA MAONI YAKO HAPA
0 comments:
Post a Comment