LOWASA KUCHUKUA FOMU ZA URAIS KATIKA OFISI ZA TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI JUMATATU, PATA MAELEZO ZAIDI
Chama  cha  Demokrasia  na  Maendeleo (CHADEMA) kimetoa taarifa kuhusu utaratibu wa Mgombea wa UKAWA, Edward Lowassa kuchukua Fomu za  Urais  katika  ofisi  za  Tume  ya  Taifa ya  Uchaguzi.
Akitoa  taarifa  hizo  mbele  ya  waandishi  wa  habari  leo  mchana, Naibu Katibu  Mkuu  wa  Chadema, ndg  Salum  Mwalimu  ambaye  kwa  sasa  anakaimu  nafasi  ya  Katibu  Mkuu  wa  Chadema  amesema  Mh. Lowassa  atachukua  fomu  hizo  Jumatatu  ya  tarehe 10, Agosti  2015, saa  tatu  kamili  asubuhi.
Mwalimu amesema msafara wa Lowassa utaanzia katika ofisi za CUF zilizopo Buguruni ambapo utaelekea ofisi za Tume ya Uchaguzi kwa ajili ya Kuchukua fomu.
Baada ya zoezi la kuchukua fomu, msafara huo utaelekea makao makuu ya CHADEMA Yaliyoko Kinondoni ambapo kutakuwa na shamrashamra kidogo.
Hapa kuna sentensi 14 ambazo mwalimu amezitamka wakati akiongea na waandishi wa habari.
1.Tupo ktk Kipindi cha Uchaguzi na Wagombea Urais wa Z'bar na TZ Bara tayari tumewatangaza'-
2.Tarehe 10 Mgombea Urais wa TZ ataongozana na Mgombea mwenza wake kwenda kuchukua Fomu NEC.
3.Mh. LOWASSA atasindikizwa na Viongozi Mbalimbali wakubwa wa Vyama vinavyounda Umoja wa UKAWA.
4.Zoezi la Uchukuaji wa Fomu msafara utaanzia Ofisi za CUF Buguruni kuelekea Tume ya Uchaguzi.
5.Msafara utaishia Ofisi za CHADEMA K'ndoni ambapo kutakuwa na shamrashamra kidogo.
6.Mh. LOWASSA atazunguka Mikoani kutafuta wadhamini, Watz wana hamu kumuona LOWASSA akiwa na combat ya CDM.
7.Mtaniwia radhi kwamba hatoweza kuzunguka nchi nzima, tutatangaza maeneo ambayo atapita.
8.Baada ya Uzinduzi wa Kampeni Dar, LOWASSA atapita Majimbo yote kama alivyoahidi.
9.LOWASSA Tarehe 13 atashiriki na Viongozi wengine kwenye Mazishi ya Mzee KISUMO Mkoa wa K'njaro.
10.Hatuwezi kuwazuia watu wanaotaka kumsindikiza LOWASSA kuchukua Fomu Ofisi za NEC.
11.Kazi ya kugawanya Majimbo ya Ubunge imekamilika, kazi imekamilika salama na kwa amani.
12.Kuna jambo linaendelea watu wanaambiwa wakusanye Kadi zao za Kupigia Kura.
13.Yoyote anayeambiwa atoe kadi au atoe namba ya Kadi yake ya Kupigia Kura akatae.
14.UKAWA haijayumba kwa namna yoyote kwa kuondoka kwa Prof. LIPUMBA, tunasonga mbele.

 Tanzanian Shilling Converter
  Tanzanian Shilling Converter

 Posts
Posts
 
0 comments:
Post a Comment