Mh. Faustine Ngugulile(mb) amemkaribisha Mh. Harrison Mwakyembe(waziri) kukagua ujenzi unaoendelea wa mahakama mpya Kigamboni leo.
Mapema mchana wa hii leo Mh. Harrioson Mwakyembe waziri wa
Katiba na Sheria ametembelea kukagua ujenzi unaoendelea wa mahakama mpya ya
Kigamboni. Mahakama hiyo iliyopo mahali ambapo ilikuwepo mahakama ya zamani ya
mwanzo Kigamboni. Mahakama hiyo kubwa na
kisasa inategemewa kuwa na kumbi za mahakama mbili na vyumba vitatu vya
kuhifadhia mahabusu na ofisi nyingine.
Mh. Fausine Ndugulile(mb) aliyekuwa mwenyeji wa Mh Waziri
Mwakyembe alitumia fursa hiyo kumuelezea Mh. Mwakyembe(Waziri) kero
zinazowakabiri wakazi wa Kigamboni kuhusiana na mahakana., zikiwemo za
ucheleweshwaji wa kesi na rushwa.
Aidha Mh. Waziri Mwakyembe alijibu kuhusiana na kero hizo na
kuelezea kuwa miaka mitatu iliyopita kulikua na asilimia sitini ya
ucheleweshwaji wa kesi, ambayo sasa imeshuka hadi kufikia asilimia kumi na
tano. Na bado serikali inashughulikia ipungue zaidi ya hapo. Alimaliza kwa
kusema kuwa serikali inategemea kuwa ndani ya miaka mitano kila kata iwe na
Mahakama yake.
Mhandisi Eng. Noel Sylvester wa kampuni ya ujenzi ya Moladi Tanzania building communities amesema kuwa ujenzi
huo utakamalika mwezi wa pili mwakaniEng. Noel Sylvestor akimuonesha Mh. Mwakyembe uimara wa kuta za jengo hilo la Mahakama
Mh Mwakyembe(waziri) akioneshwa ramani ya jengo hilo la Mahakama
Mh. Faustine Ndugulile(mb) akionesha ramani na Mhandisi Eng. Noel Sylvester
Mh. Mwakyembe(waziri) akionesha picha ya mahakama hiyo itakavyokua
Mh. Harrison mwakyembe(Waziri) akiagana na Mh. Faustine Ndugulile baada ya kumaliza shughuli ya ukaguzi wa uujenzi wa mahakama hiyo ya Kigamboni
0 comments:
Post a Comment