Ommy Dimpoz aeleza kwanini alisita kuingiza sokoni mavazi ya PKP (Video)
Kuna wakati Ommy Dimpoz aliwahi kuahidi kuwa angeingiza sokoni mavazi ya brand yake ya PKP na aliwahi kutengeneza hadi sample zake.
Lakini hadi sasa, hakuna dalili kuwa mavazi hayo yatazinduliwa rasmi.
Akiongea na Bongo5, Ommy amesema alisita kuingia kichwa kichwa kwenye biashara hiyo sababu aligundua atawanufaisha wajanja wachache.
Ommy anadai kuwa kuna wafanyabiashara kibao ambao wanasubiri mastaa waanzishe brand zao na kisha kwao kwenda kutengeneza makontena ya mzigo China na kuuza kwa bei nafuu.
0 comments:
Post a Comment