Advertise with us here... Contact: 0654 264 472 Email: sabanhussein@yahoo.com sabanhussein@yahoo.com

Thursday, April 27, 2017

MICHEZOTazama matokeo ya mechi za EPL zilizochezwa Jumatano

Usiku wa Jumatano, zilichezwa michezo mitatu ya ligi kuu ya Uingereza – Arsenal, huku wakiwa katika uwanja wao wa nyumbani wa Emirates walifanikiwa kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Leicester City. Beki Robert Huth wa Leicester alijifunga goli hilo katika dakika ya 86 ya mchezo huo.
Katika mchezo mwingine, Criystal Palce waliokuwa katika uwanja wao wa nyumbani wa Selhurst Park walijikuta wakiangukia pua, mbele ya Tottenham Hotspur kwa kufungwa goli 1-0. Goli la Spurs lilifungwa na kiungo wao Christian Dannemann Eriksen katika dakika ya 78.

Nao Sunderland wakiwa katika uwanja wa ugenini wa Riverside Stadium wa Middlesbrough, walifungwa bao 1-0. Bao hilo pekee la Middle lilifungwa na Marten de Roon kwenye dakika ya nane ya mchezo huo.
Wakati huo huo, mechi kubwa inayosubiriwa kwa hamu leo (Alhamisi) ni kati ya Manchester City ambao watawakaribisha majirani zao Man United katika uwanja wa Etihad.

0 comments:

Post a Comment

Total Pageviews

Popular Posts

Unordered List

http://michuzijr.blogspot.com/2013/03/party-kubwa-ya-pasaka-kudondoshwa.html

Flickr Images

Follow Us

Bin Hussein65 copyright 2014. Powered by Blogger.

Translate

Followers

Search This Blog