Advertise with us here... Contact: 0654 264 472 Email: sabanhussein@yahoo.com sabanhussein@yahoo.com

Thursday, April 27, 2017

Watanzania ni wakosoaji sana – Quick Rocka

Msanii wa muziki na mtayarishaji, Quick Rocka ‘Switcher’ amedai watanzania wengi wana tabia ya kumsubiri mtu akosee ili wamseme vibaya na sio wepesi kushauri mapema.
“Watanzania wengi ni wakosoaji. Wasanii wengi wanaoharibu kazi huwa wanawaogopa wakosoaji na ndiyo maana utakuta wanahangaika kutengeneza muziki wa tofauti kumbe ndiyo wanaharibu,” Rocka alikiambia kipindi cha Planet bongo ya EA Radio.
Aliongeza, “Mimi nawashauri tu kama watu wanataka muziki mzuri wasikilize nyimbo za zamani kisha wakitengeneze kazi zao yani hit song,”
Katika hatua nyingine, Quick Rocka amesema wimbo wake mpya aliyomshirikisha Mimi Mars ni mchanganyiko wa nyimbo nyingi ukiwemo wa ‘One dance’

0 comments:

Post a Comment

Total Pageviews

Popular Posts

Unordered List

http://michuzijr.blogspot.com/2013/03/party-kubwa-ya-pasaka-kudondoshwa.html

Flickr Images

Follow Us

Bin Hussein65 copyright 2014. Powered by Blogger.

Translate

Followers

Search This Blog