Advertise with us here... Contact: 0654 264 472 Email: sabanhussein@yahoo.com sabanhussein@yahoo.com

Monday, February 20, 2017

Fid Q akaribia kuachia kitabu chake cha kwanza ‘The Swahili Kid’

Mbali na kuwa na misemo migumu ya kumfanya mtu kutumia muda mwingi kusikiliza kwa umakini mashairi ya nyimbo zake, sasa rapper Fid Q ameingia kwenye uandishi wa vitabu.
Rapper huyo ameiambia Bongo5 , kitabu chake hicho cha kwanza kinaitwa ‘The Swahili Kid’ na kitatoka baada ya albamu yake ya tatu Kitaaolojia.
“Nina kitabu kizima ambacho kinakuja kinaitwa ‘The Swahili Kid’. Ambacho kinasubiriwa kama inavyosubiriwa albamu yangu ya tatu ‘Kitaaolojia’. Kwenye kitabu hicho nimechambua kuanzia albamu yangu ya kwanza, ya pili na mpaka hii ya tatu. Kinachelewa kutoka kwa sababu sasa hivi nipo kwenye albamu yangu ya tatu ‘Kitaaolojia’,” amesema Fid.
Rapper huyo ameongeza kitabu hicho kitatoka pindi albamu yake hiyo ya tatu itakapotoka Agosti 13 ya mwaka huu.

Related Posts:

0 comments:

Post a Comment

Total Pageviews

273585

Popular Posts

Unordered List

http://michuzijr.blogspot.com/2013/03/party-kubwa-ya-pasaka-kudondoshwa.html

Flickr Images

Follow Us

Bin Hussein65 copyright 2014. Powered by Blogger.

Translate

Followers

Search This Blog