HIVI UNAJUA T.SHIRT YA DIAMOND NA DEMU ALIYE VAA BIKINI KWENYE VIDEO YA "KABINTI SPECIAL" YA DULLY NDIO WALIOSABABISHA VIDEO IFUNGWE!!! SOMA ZAIDI
Msanii mkongwe wa muziki nchini, Dully Sykes amesema miongoni mwasababu zilizofanya BASATA ifungie video yake ya ‘Kabinti Special’ ni mwanamke aliyevaa mavazi tata ya kuogelea pamoja na t-shirt ya Diamond yenye matusi.
Akizungumza na Clouds FM, Dully alisema:
Video yangu imefungiwa wanasema kwaajili ya maadili ,wanasema sijui Diamond amevaa fulana sijui wameandika sijui nini na video queen sijui amevaa swimming costume nguo ambazo hazipo kimaadili. Unajua sisi Watanzania tukifanya hivi kila siku tutakuwa hatuna maendeleo kwasababu ukiangalia South Africa uchumi wao unapanda kwajaili ya muziki. Pia unachangia muziki kupanda. Nigeria pia unachangia muziki kupanda, muziki umepanda na uchumi umepanda pia hata Kenya hapo. Pia hata Uganda kwaajili wao wanamuziki wanafanya uchumi upande na nchi yao inapendeza kuona kwamba ina mastaa wazuri ambao wanafanya kazi nzuri kupigwa katika nchi zote duniani na kujulikana. Unajua msanii anapojulikana ametoka nchi fulani,mtu mwingine Tanzania haijui akimuona lakini amemuona Tunda amemuona katika MTV anajua kuna nchi inaitwa Tanzania, kwahiyo sisi Watanzania na serikali inabidi ikae chini tuangalie tukitaka kuleta mambo ya maadili kila siku tutakuwa nyuma kila siku inabidi tuendelee mbele kama wao wanavyoweza kujenga barabara zenye lami kila sehemu kama kuiga wenzetu nchi iwe na maendeleo na sisi tunataka watuachie tuangalie maendeleo ya sisi wanamuziki tunafika wapi,tunabidi na sisi siku moja tuwe na sehemu zetu kubwa. Sasa wakitaka basi mtu akivaa swimming costume, hayupo mtupu anataka video isipigwe.”
Dully alisema hii ni mara ya pili kwa wimbo wake kufungiwa.
“Hii mimi si mara ya kwanza kwasababu ata Nyambizi waliifungia. Kwakweli mimi walivyonikatisha tamaa ile sikutaka tena kuendelea nikasema ngoja niangalie kitu kingine cha kufanya. Yeah kwasababu kama nchi yangu inanikatisha tamaa, nchi gani itakuja kunisupport? Kiukweli kabisa mimi naongea kama kiongozi wa wana bongo flava Tanzania muziki wa kuimba,” alisema.
“Serikali inabidi ituangalie sisi tunafanya muziki ili kupandisha nchi yetu ili iwe kwenye nafasi nzuri. Kiukweli kabisa wanabidi watuachie ili tufanye kazi ili kuisaidia nchi yetu kufika mbali. Sasa wanawake wakiwa wanavaa madila kwenye nyimbo za kisasa sasa itakuwaje?”

0 comments:
Post a Comment