Advertise with us here... Contact: 0654 264 472 Email: sabanhussein@yahoo.com sabanhussein@yahoo.com

Thursday, December 8, 2016

Gigy Money azungumzia malezi aliyokulia, kucheza kamari, pamoja na utangazaji ulivyobadili maisha yake (Video)

Video Vixen Gigy Money Jumatano hii alitembelea Bongo5 na kufunguka mambo mengi kuhusu maisha yake pamoja na jinsi kazi yake mpya ya utangazaji ilivyobadili maisha yake.



“Mimi ndo mtoto ambaye nimekaa na mama muda mrefu na mama nilikuwa namchefua, alikuwa anaona sina faida, anasema baba yako amekukataa bado unaning’ang’ania. Ila mimi nilikuwa naonyesha upendo, sio kama nilikuwa namsumbua nilikuwa nampenda sana, sema nilikuwa natafuta hela,”
“Kiukweli nimecheza kamari nikiwa mdogo sana, kama darasa la tatu la nne hivi, na nilikuwa na bahati sana ya kula, mtu alikuwa yupo radhi anikopeshe hela yake nicheze kwa sababu anajua nitakula, lakini hela zote nilikuwa naenda kumpatia Mama. Kwahiyo nikajikuta maisha yanakuwa marahisi sina mpango wa wanaume lakini hela napata. Lakini ikafika hatua mama akaona tunaenda kuaharibikiwa kwa hiyo akaanza kutukataza, nikapigwa sana kuacha kamari,” aliongeza Gigy Money.
Pia Gigy amedai kazi yake mpya ya utangazaji imeanza kubadili maisha yake pamoja na kumfanya atafute njia mpya za kuingiza pesa kupitia brand yake aliyoitenga kwa miaka mingi.

0 comments:

Post a Comment

Total Pageviews

Popular Posts

Unordered List

http://michuzijr.blogspot.com/2013/03/party-kubwa-ya-pasaka-kudondoshwa.html

Flickr Images

Follow Us

Bin Hussein65 copyright 2014. Powered by Blogger.

Translate

Followers

Search This Blog