Ndoa ya Kanye West na mkewe Kim Kardashian yaelekea ukingoni
Mwisho wa ndoa ya Kanye West na Kim Kardashian wanukia baada ya kudumu kwa zaidi ya miaka miwili na nusu.
Tovuti ya Us Weekly imeripoti Jumatano hii kuwa Kim hana furaha ndani ya ndoa yake hivyo amepanga kudai talaka pindi Kanye atakaporudi kwenye hali yake ya kawaida.
Imedaiwa kuwa mrembo huyo amepanga kufungua kesi hiyo ya kudai talaka pamoja na kupatiwa haki zote za malezi ya watoto wao wawili, North na Saint.
Kwa sasa Kanye West anaishi nyumba tofauti na mkewe Kim Kardashian na wanae. Lisemwalo lipo na kama halipo basi linakuja.
0 comments:
Post a Comment