Kituo cha kusaidia watoto yatima cha Amani Foundation For Orphanage kimepata mkono wa sikukuu
Kituo cha watoto yatima cha Amani Foundation for Orphanage kimetembelewa na Mh. Faustine Ndugulile(Mb), Uhuru Music(T) Limited na Dege stationary na kupatiwa zawadi mbalimbali siku ya leo. Kituo hicho kilichopo Ungindoni kata ya Mjimwema chenye watoto yatima 35 wanaolelewa kwenye kituo hicho wakiume na wakike. Kituo kilianzishwa mwaka 2014 kikiwa na watoto 12 huko Kisota Kigamboni, na baadae kuhamia Ungindoni Mjimwema, Kigamboni ambapo kipo hivi sasa.
Mh. Faustine Ndugulile aliwakaribisha Uhuru Music.Tanzaia Limited na Dege Stationary kutembelea kitu hicho ambacho miezi kadhaa iliyopita kilivamiwa na wezi walioiba baadhi ya vitu muhmu katika kituo hicho. Vitu hivyo vilivoibiwa vikiwemo sare za shure za watoto, vyakula n.k.
Vitu vyote vilivyokabiziwa na Uhuru Music (T) Limited na Dege Stationary vina thamani ya Tsh MIlioni 3.
Baadhi ya watoto wanaoishi katika kituo cha Amani Foundation for Orphanage
Mh. Faustine Ngugulile(Mb) akiambatana na watoto wake akiwasilisha zawadi zake
Watoto wa kituo hicho wakisaidia kushusha zawadi zao
Mlezi wa kituo hicho Hayjat Zubeyda Abdallah akielezea kuhusu kituo
Mtoto Juma Nassoro anayelelewa katika kituo cha Amani Foundation for Orphanage akisoma Risala mbele ya Mgeni rasm Mh. Faustine Ndugulile(Mb)
Mtoto Juma Nassoro anayelelewa katika kituo cha Amani Foundation for Orphanage akikabidhi Risala mbele ya Mgeni rasm Mh. Faustine Ndugulile(Mb)
Inspekta Fatuma wa kutoka dawati katika kituo cha polisi Kigamboni, aliyemuwakilisha OSD mkuu wa polisi wilaya ya Kigamboni akieleze masikitiko yake kutokana na uhalifu uliyotokea katika kituo hicho
Mh. Faustine Ndugulile(Mb)
Bw. Sanga Mkurugenzi wa Uhuru Music (T) Limited akielezea alivyoguswa kutembelea na kusaidia kituo cha Amani Foundation for Orphanage
Mkurugenzi wa dege stationary nayeye alipata nafasi ya kuelezea alivyoguswa kutembelea kituoni hapo
Watoto wa Mh. Ndugulile(mb) waliongozana na baba yao kutembelea na kukabidhi zawadi kwa watoto wenzao wanaolelewa katika kituo cha Amani Foundation for Orphanage
Nelvin Ndugulile mtoto wa Mh. Ngugulile(Mb) akikabidhi zawadi ya Vitabu mbalimbali kwa watoto wenzake
Martha Ndugulile, mtoto wa Mh. Ndugulile nayeye akikabidhi zawadi zake
Mkurugenzi wa Uhuru Music (T) Limited akimjaribisha mtoto mmoja shati la shule, ni miongoni mwa zawadi ambazo wamewazawadia watoto hao
0 comments:
Post a Comment