Advertise with us here... Contact: 0654 264 472 Email: sabanhussein@yahoo.com sabanhussein@yahoo.com

Sunday, February 26, 2017

UDSM chapinga kudahili wanafunzi vilaza

Siku moja baada ya Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) kutangaza utata wa udahili wa wanafunzi wa vyuo vikuu, wadau wakubwa wa elimu, wamejitokeza kupinga hatua hiyo. Wadau hao ni pamoja na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) na Baraza la Vyuo vya Ufundi Tanzania (NACTE).
Taarifa ya chuo kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) kwa upande wake kimeeleza kwamba hakuna mwanafunzi hata mmoja aliyedahiliwa chuoni hapo, ambaye hana sifa za kujiunga na chuo hicho.
Naibu Makamu Mkuu wa Chuo hicho, Profesa Florens Luoga aliliambia gazeti la habarileo Alhamisi hii kuwa chuo hicho kimeweka utaratibu ambao unaweza mwanafunzi yeyote anayedahiliwa chuoni hapo, awe na sifa zinazohitajika kwa kuwa hawafanyi biashara.
Alisema Luoga, “Sisi hapa ni wakali kuhusu jambo hilo, tukibaini kuwepo kwa mwanafunzi ambaye hana sifa tunamfukuza. Hatusubiri TCU iseme, hata tukibaini kuwa mtu alifanya udanganyifu na alishamaliza chuo, lakini hakuwa na sifa, tunamnyang’anya digrii tulivyompa.”
Aliongeza kuwa, “Hiki ni chuo, hatufanyi biashara, sisi kazi yetu hapa ni kuandaa wataalamu na ndio maana tunakuwa wakali na makini kuhakikisha wanafunzi tunaowachukua, wote wanakuwa na sifa stahiki.”
Aidha Luoga alisema chuo hicho kikongwe Tanzania, kutokana na kuwepo makubaliano hayo kimekuwa kinapokea baadhi ya wanafunzi ambao wanatoka nje ya nchi na akasisitiza kuwa yawezekana ndio hao ambao TCU imeshindwa kupata nyaraka zao.
By: Emmy Mwaipopo

0 comments:

Post a Comment

Total Pageviews

Popular Posts

Unordered List

http://michuzijr.blogspot.com/2013/03/party-kubwa-ya-pasaka-kudondoshwa.html

Flickr Images

Follow Us

Bin Hussein65 copyright 2014. Powered by Blogger.

Translate

Followers

Search This Blog